Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga chuo kikubwa Cha Uhasibu CBE Kampasi ya Kilimanjaro. Amesema Chuo hicho kitakachojengwa wilayani Hai mkoani humo kitasaidia kuchochea uchumi wa wananchi. Aidha, DKT. Samia amesema kuwa endapo Wananchi watampatia ridhaa ya kuongoza tena Nchi kwa kumchagua katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu watajenga barabara ya mchepuko Bypass ya Kahe - Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Ametoa ahadi hizo alipokuwa akijinadi katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye Uwanja wa Mashujaa Moshi Mjini leo Oktoba Mosi, 2025.
- Get link
- X
- Other Apps